NMB YAWAFIKIA WANA KONGWA: YAFUNGUA TAWI JIPYA KIBAIGWA-KONGWA, DODOMA

NMB leo imefungua tawi jipya katika mji maarufu wa Kibaigwa �Dodoma. Tawi hilo litakuwa na huduma zote za kibenki kama yalivyo matawi mengine ya NMB nchini kote. Tawi la Kibaigwa limefunguliwa na Naibu spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa Kongwa, Mh Job Ndugai. Kufunguliwa kwa tawi la Kibaigwa kunafuatia mahitaji ya muda mrefu ya wateja wa NMB wa eneo hilo wa kupata tawi lenye nafasi ya kutosha .Aidha eneo hili ni karibu zaidi na wafanyabiashara wengi ambao ni wateja wakubwa wa NMB na wananchi kwa ujumla . Kwa kutambua pia nia ya kuendelea kuchangia huduma mbali mbali za kijamii, benki ya NMB inatoa shilingi Milioni 10 kwa ajili ya hospitali na shule kama shukrani za Benki kwa wananchi wa Kibaigwa kwa kuendelea kwao kuunga mkono maendeleo ya benki. NMB ndiyo benki inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi zaidi ya 150, ATM Zaidi ya 500 nchi nzima pamoja na idadi ya wateja inayofikia Milioni mbili hazina ambayo hak...