DIAMOND AKIRI KUTOKUMUOA WEMA....sikia alichosema wema
KAULI ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul �Diamond Platnumz� kwamba hawezi kuoa kamwe, inadaiwa kumchefua mwandani wake, Wema Isaac Sepetu �Beautiful Onyinye�, Amani limenyetishiwa. Wema Sepetu akiwa na Nasibu Abdul �Diamond Platnumz�. Aliporejea Bongo kutoka Marekani juzikati, Diamond alitoa kauli hiyo na kuandikwa kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti dada la hili, Ijumaa, toleo la wiki iliyopita likiwa na kichwa cha habari; �DIAMOND: SITAOA KAMWE� ambapo ndani yake alieleza jinsi ambavyo mastaa wengi waliooa wameanguka kisanii. MTU WA KARIBU AYASEMA YA WEMA Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao, Wema hakufurahishwa na habari hiyo kwa sababu anajua yeye ndiye mke mtarajiwa wa Diamond. Ilidaiwa kwamba, Wema alijikuta akipoteza ile furaha ya kwamba wawili hao wangefunga ndoa mwezi huu (Agosti) kama ilivyotabiriwa na mnajimu maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein. �Baada ya kauli hiyo ya Diamond na kutotimia kwa utabiri wa Maalim Hassan ...