Posts

Showing posts with the label BONGO MOVIES

Kuna ukweli wowote hii ishu ya Director wa Bongo Movie kumwingilia kinguvu mwigizaji?? #UHeARD

Image
Hii ishu imefika mezani kwa gossip cop  Soudy Brown  .. inahusu mwanafunzi ambae amelalamika kwamba ilikuwa mara yake ya kwanza kuigiza, ikatokea director mmoja wa bongo movie akamwingilia kinguvu. Dadake msichana huyo amesimulia kwamba walikuwa location kufanya movie, director huyo akamuita mdogo wake kwenye chumba chake na kumwingilia kwa nguvu. Msichana aliyefanyiwa kitendo hicho amesema hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuigiza.. siku ya tukio walikuwa location, director huyo akamuita kwenye chumba cha wanaume ili amuelekeze kitu, alipoingia akamfanyia kitendo hicho.. alijaribu kupiga kelele lakini watu hawakusikia na alishindwa kutoa taarifa kwa kuhofia kupata aibu. Kusikiliza stori yote bonyeza play hapa chini�

Picha: Mtoko wa Pasaka wa Irene Uwoya Huko Mwanza

Image
Hizi ni baadhi ya picha ambazo staa mrembo Irene Uwoya ame-share nasi kupitia ukursa wake kwenye mtandao wa Instagram akiwa jijini Mwanza ambako amekwenda kikazi zaidi. Huu ndio ulikuwa mtoko wake wa sikukuu ya PASAKA hapo jana. Mbali ya picha hizi kusababisha mafuriko ya LIKES na COMMENTS huko Instagram, Sio mbaya nawewe hapa kama mdau ukasafisha macho na picha hizi na kufunguka chochote kuhusu mtoko huu wa mrembo huyu ambae anatajwa kama ni mmoja kati waigizaji wa rembo zaidi hapa Bongo. Kwa upande wangu Irene ndio staa alitokelezea bomba zaidi kwa siku ya jana. Umependeza sana Uwoya.

Hekaheka ya leo inamhusu muigizaji maarufu aliyesingiziwa mtoto. #Hekaheka

Image
Hekaheka ya leo muigizaji maarufu Single Mtambalike maarufu kama Richie, ameelezea hekaheka yake ya kusingiziwa Mtoto na mwanamke kutoka Shinyanga ambaye alifika nyumbani kwake akiwa na mtoto mchanga na kudai ni mtoto wa msanii huyo. Richie amesema wakati huo ndoa yake ilikuwa changa na mke wake alikuwa na mtoto mchanga kitendo ambacho kiliitikisa ndoa yake. Jamaa anasema hakuwahi kumwona mwanamke huyo, hivyo baada ya kukasirishwa na kitendo hicho alijikuta akimpiga mwanamke huyo makofi. 96.0 Clouds Fm inasikika ukiwa Tanga. Hapa unaweza kuisikiliza Hekaheka yote kwa kubonyeza play.