Posts

Showing posts with the label Michezo

Mourinho:Taji la mchezaji bora lifutwe

Image
  Kocha wa Chelsea Jose Mourinho    Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho anaamini kwamba taji la mchezaji bora duniani Ballon d'Or linafaa kuondolewa. Mourinho anasema kuwa lengo la soka linabadilika kutoka timu za soka hadi kwa wachezaji binafsi. ''Tuanaangazia mchezo wa mchezaji mmoja, pasi alizotoa na amekimbia kilomita ngapi uwanjani.Pengine ulikimbia kilomita 11 na mimi nilikimbia kilomita tisa,lakini kilomita zangu zilikuwa muhimu kushinda zako'',alisema Mourinho. Amesema kuwa Chelsea boss Jose Mourinho believes the Ballon d'Or should be scrapped. Je, unadhani FIFA inafaa kulifutilia mbali taji la mchezaji bora duniani.Ingia katika mtandao wetu wa facebook katika bbcswahili uweke maoni yako.

Fifa yatoa viwango vipya vya soka .

Image
  Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) limetoa viwango vipya vya soka duniani huku Tanzania na Rwanda zikishuka kwa nchi za Afrika ya Mashariki wakati Kenya, Uganda na Burundi zikipanda viwango. Kushuka na kupanda kwa viwango kunatokana na mechi za kirafiki za kimataifa za Fifa zilizofanyika mwezi Machi , ambazo matokeo yake ni sehemu ya kigezo. Tanzania, baada ya kutoka droo ya 1-1 na timu ya Malawi katika moja ya mechi hizo za kirafiki, imeshuka kutoka nafasi ya 100 mpaka ya 107 huku Rwanda ikishuka nafasi 10 hadi ya 74 baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Zambia cha magoli 2-0 mwezi Machi. Uganda ndio nchi inayoongoza katika Afrika ya Mashariki ikipanda nafasi mbili juu na kushika nafasi ya 72 baada ya kuwafunga Nigeria 1-0. Burundi nayo imepanda kutoka nafasi ya 126 mpaka ya 123 mbali ya kutoka droo ya 2-2 na timu ya Mauritius. Kenya pia imepanda nafasi moja juu na sasa ipo ya 117 huku ikiwa na rekodi ya kuifunga Shelisheli 2-0 katika mechi yake ya kirafiki. ...

Kusuka au kunyoa Twiga au Shepolopolo?

Image
Shepolopolo    Ni kusuka au kunyoa ambapo kitendawili cha timu gani itafuzu kucheza fainali za michezo ya Afrika kwa upande wa soka la wanawake kati ya wenyeji Twiga Stars au Shepolopolo ya Zambia kitatenguliwa pale timu hizo zitakapokwaana katika mechi ya kufuzu Ijumaa jijini Dar es Salaam. Kuelekea katika mchezo huo, makocha wa timu zote wametambiana huku kocha mwenyeji, Rogasian Kaijage wa Twiga Stars akijivunia kuwa uwanja wa nyumbani ambapo robo tatu ya mashabiki watakuwa upande wake. Kaijage na nahodha wake Sophia Mwasikili wamewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuja kuwashangilia. Kocha wa Shepolopolo, Albert Kachinga, akiwa nyuma ya magoli 2-4 katika mchezo wa kwanza uliochezwa mjini Lusaka, amesema amefanyia kazi makosa yaliyosababishwa kufungwa na wana matumaini ya kushinda. Zambia pia ina nafasi endapo itaifunga Stars kwa zaidi ya idadi ya magoli yale ya awali waliofungwa nchini mwao. Mechi inatarajiwa kuanza majira ya saa 10...

Taifa stars ya Tanzania yajinasibu

Image
  Kocha wa Taifa Stars Mart Nooij Licha ya kupangwa katika kundi gumu na timu za Nigeria, Misri na Chad katika michuano ya kuwania kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 nchini Gabon, kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mdachi Mart Nooij amesema timu yake haiziogopi timu hizo. Ameongeza kuwa badala yake, zitegemee pia upinzani mkali kutoka kwa Stars ambayo ana amini itakuwa imejiandaa vema kwa ajili ya mashindano hayo ambapo kushinda, kufungwa au kupata sare itakuwa ni sehemu ya matokeo. Michuano ya Cosafa itakayofanyika nchini Afrika ya Kusini siku chache zijazo itakuwa ni sehemu ya maandalizi kwa Stars, kwa mujibu wa Nooij, ambaye anasema Stars itahitajika kutoa ushindani mkubwa. kikosi cha Taifa stars    Taifa Stars itakuwa na kibarua kigumu katika kugombea nafasi mbili kwa ajili kwenda kucheza fainali. Stars imeshuka katika viwango vya FIFA vya mwezi April vilivyotolewa Alhamis kutoka nafasi ya 100 mp...

Djokovic aendelea kung'ara

Image
  Novak Djokovic ameendelea kuongeza mataji ya mchezo huo na sasa yamefikia saba. Hatua hiyo imekuja baada ya jana kunyakua ubingwa michuano ya Miami Open kwa kumbwaga mpinzani wake Andy Murray. Ubingwa huyo namba moja kwa ubora duniani alimbwaga mpinzani wake kwa seti 7-6 ,7-3, 4-6, 6-0. Na baada ya mechi za jana za ligi kuu ya England leo kutakuwa na mchezo mmoja ambapo Crystal Palace watawakaribisha Manchester City.

CAF:Morocco kushiriki katika michuano

Image
  Shirikisho la soka barani Africa CAF limethibitisha kuwa Morocco itashiriki katika mechi za kufuzu kwa dimba la Afrika mwaka 2017. Siku ya alhamisi mahakama ya kusuluhisha mizozo ya michezo Cas ilibadilisha marufuku iliowekwa na CAF dhidi ya Morrocco ya kutoshiriki michuano ya mwaka 2017 na 2019. Lakini siku ya ijumaa mkurugenzi wa mawasiliano wa CAF Junior Binyam aliiambia BBC kwamba kuna mikutano mingi itakayofanywa kabla ya uamuzi kufanywa. ''Tusubiri kitakachofanyika'',alisema.Droo ya mechi za kufuzu inatarajiwa kufanyika tarehe 8 mwezi Aprili. Siku ya jumapili,Shirikisho la soka barani CAF lilitanagaza kuwa lilikubali uamuzi uliofanywa na mahakama hiyo kufuatia mkutano mkuu wa kamati ya mahakama hiyo huku ikitoa sababu zao katika mtandao.

JAJA,MSUVA KUNG'AA KWENYE MECHI YA NGAO YA JAMII UWANJA WA TAIFA LEO

Image
Jaja aliingia �mzima mzima� pembezoni mwa lango la Thika kuhakikisha anaiunganishia nyavuni krosi ya Msuva kwa vyovyote na akafanikiwa akimuacha kipa Mganda, Hamza Muwonge anaokota mpira nyavuni. Kwa furaha ya bao hilo, Jaja ambaye alikuwa akizomewa na mashabiki wa Simba SC kila alipokosea alitoka nje ya Uwanja kushangilia bao hilo, kwa shangwe za aina zote alizoweza. Yanga SC haikucheza vizuri kipindi cha kwanza na zaidi ilitegemea kupitisha mashambulizi yake pembeni walipokuwa wakiteleza kwa awamu Simon Msuva, Haruna Niyonzima na Andrey Coutinho. Coutinho alikaribia kufunga mara mbili kwa mipira ya adhabu aliyopiga kutoka nje kidogo ya eneo la penalti, wakati Jaja hakuwa na madhara kabisa kipindi cha kwanza. Nafasi nzuri zaidi kwa Thika ilikuwa dakika ya 20 wakati shuti la Moses Odhiambo lilipodakwa na kipa Deo Munishi �Dida�- zaidi ya hapo, safu ya ulinzi ya Yanga SC leo ilicheza vizuri. Kipindi cha pili, kocha Mbrazil Marcio Maximo alianza na mabadiliko katika safu ...

YANGA SPORTS CLUB KUIVAA AZAMA FC LEO TAIFA

Image
 KIKOSI KAZI CHA YANGA FC KIKOSI KAZI CHA AZAM FC NGAO YA JAMII mabovu story .com ndio mtandao wako kwa habari za burudani Africa na nje, Tuwe pamoja huku pia  >> Instagram , Twitter Na Facebook

Alichosema Cristiano Ronaldo baada ya Falcao kuhamia Man United

Image
Usiku wa jana klabu ya Manchester United ilikamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao kwa mkopo. Falcao ambaye alikuwa akiwindwa na vilabu vya Arsenal na Man City amejiunga na Man U akitokea klabu ya Monaco ambayo alijiunga nayo akitokea Atletico Madrid. Usajili wa mchezaji umezungumzia na watu wengi mmoja wao ni mchezaji bora wa ulaya na dunia � Cristiano Ronaldo. Akiongea jijini Madrid Ronaldo alisema: �Falcao ni mchezaji mzuri sana, nadhani Manchester United wamefanya jambo zuri kumsajili. Sidhani kabisa kama ni mchezaji asiyewafaa, ni mchezaji wa daraja la dunia na hivyo naamini huu usajili mzuri.�

Unaambiwa Man United wamekamilisha usajili mwingine wa huyu Muargentina.

Image
Baada ya usajili wa Ander Herrera na Luke Shaw, Manchester United wamekamilisha usajili wa mchezaji mwingine ambae ni Marcos Rojo, beki wa kiargentina aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Sporting Lisbon. Rojo ambaye alichaguliwa katika kikosi bora cha kombe la dunia, amejiunga na United kwa ada ya uhamisho wa �16 pamoja na Luis Nani kwenda Sporting kwa mkopo ambapo pia Manchester United wanaripotiwa kuhamishia nguvu zao kwa Angel di Maria wa Real Madrid.

Usajili wa Luis Suarez FC Barcelona na rekodi mpya ya gharama za usajili

Image
Baada ya uwepo wa tetesi za kuihama Liverpool kushika hatamu kwa takribani wiki 3 sasa, hatimaye leo hii Luis Suarez amejiunga rasmi na FC Barcelona akitokea Liverpool. Usajili wa Suarez umeigharimu FC Barcelona kiasi cha �65m kwa mujibu wa mtandao wa Barcelona, na hii ni rekodi kwa Liverpool � Suarez anakuwa mchezaji aliyeuzwa kwa fedha nyingi zaidi na klabu hiyo iliyoshika nafasi ya pili kwenye EPL msimu uliopita. Suarez ambaye alijiunga na Liverpool akitokea Ajax, pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji anayeshika nafasi ya nne kwa kusajiliwa kwa fedha nyingi zaidi nyuma ya Bale, Ronaldo na Neymar. Hata hivyo pamoja na usajili huo mchezaji huyo hatoweza kuitumikia Barca mpaka adhabu yake ya kufungiwa mechi 8 na kifungo cha miezi 4 kitakapoisha.

Cheki mapenzi ya shabiki huyu mwenye umri mdogo kwa mchezaji Neymar

Image
Ukizungumzia taifa ambalo limetoa mastar kadhaa wa soka Duniani hutoacha kulitaja Brazil hii ni kufuatia rekodi zake kadhaa ambazo limewahi kujiwekea kwenye medali ya soka duniani leo limeingia kwa headline tena taifa hili. Ni kuhusu mtoto mdogo amabye kwa kumtazama anaweza kuwa na umri usiozidi miaka 3,amekua ni miongoni kati ya walioumizwa na taarifa za kidaktari zinazomhusu mchezaji Neymar kuwa hatocheza mechi nyingine za Kombe la Dunia.   Kama unakumbuka Neymar alipata majeraha baada ya kuumia kwenye mechi iliyochezwa kati ya Brazil na Colombia na katika mechi hiyo Brazil ilifanikiwa kushinda goli 2-1 na kufanikiwa kuingia nusu Fainali. July 08 Brazil ambao kimsingi ndio wenyeji wa mashindano haya ya kombe la dunia itacheza na Ujeruman,mchezo utakaochezwa bila Neymar katika mechi ya Nusu Fainali.

Timu ya Algeria imerudi nyumbani kutokea kombe la dunia, hapa kuna picha 5 za jinsi walivyopokelewa

Image
Kwenye kombe la dunia linaloendelea nchini Brazil, Algeria kutoka Afrika wameingia kwenye headlines zenye rekodi za kudumu kutoka kwenye mashindano haya baada ya kuwa moja ya timu mbili za Africa zilizogusa kwenye hatua nzuri kabla ya kutolewa.   Tayari timu hii imerejea nyumbani Afrika ambapo kiukweli imepokelewa kwa shangwe sana, na naamini hata wengine wasio Waalgeria wangeipokea timu kama hii kutokana na ilichofanya.        

Kuhusu kundi la wahalifu linalouza tiketi za kombe la dunia kinyume cha sheria Brazil.

Image
Jeshi la polisi nchini Brazil limesema kuwa linawashikilia watu 11 ambao wametengeza kundi linalojihusisha na uuzaji wa tiketi za kombe la dunia kinyume cha sheria. Mtandao huo unadaiwa kuwa limejipatia fedha kinyume cha sheria kwa kuuza tiketi na tayari wamefanya uhalifu huo katika viwanja vinne vya kombe la dunia. Baadhi ya tiketi hizo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya wadhamini wakati nyingine zikiwa zimewekwa kwa ajili ya maafisa wa timu ya Brazil. Polisi wanaamini kuwa baadhi ya tiketi zimeuzwa kwa watalii wa kigeni.