Posts

Showing posts with the label BARUA NZITO

BARUA NZITO KWA MSANII WA ORIJINO KOMEDI BONYEZA HAPA USOME

Image
KWAKO, Emmanuel Mgaya �Masanja�. Naamini u mzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Kwa upande wangu nipo sawa, nakimbizana na maisha. Nina machache ya kukushauri kuhusiana na maisha yako kama staa ambaye kwa sasa umetangaza kuokoka. Kwa maneno mengine ni kwamba, umeondoka kwenye utaifa, upo mikononi mwa Muumba wako.Nimekufahamu kwa kitambo kidogo. Kwangu mimi, wewe ni mmoja wa mastaa wa ukweli katika uchekeshaji Bongo. Mwenye kipaji cha hali ya juu na unayejua unachokifanya. Tatizo ni kwamba, nashangazwa na aina ya maisha yako baada ya kutangaza kuokoka. Ninavyojua mimi, kuokoka ni kuachana na maisha ya awali ambayo (pengine) yalikuwa hayampendezi Mola na kugeukia katika maisha safi.Niliposikia umeokoka nilifurahi kuona kuwa umeelekea sehemu sahihi zaidi kiimani. Lakini moyoni nilikuwa na shaka kidogo maana wapo wasanii wengi kwenye uigizaji ambao walitangaza kuokoka lakini baadaye wakaonekana kwenye njia zao za awali. Ukiachana na waigizaji, pia kuna was...