Posts

Showing posts with the label SIASA

Iran yataka vita dhidi ya Houthi kukoma

Image
  Rais Hassa Rouhani wa Iran    Rais wa Iran Hassan Rouhani, ametoa wito wa kusitishwa kwa mashambulio dhidi ya wapiganaji wa Kihouthi nchini Yemen, akiyataja kama makosa makubwa. Iran pia imepinga madai ya Saudi Arabia kuwa utawala wa Tehran unawapa wapiganaji hao wa Kihouthi ambao ni wa shia mafunzo ya Kijeshi. Balozi wa Saudi Arabi mjini Tehran, alishutishwa kufika mbele ya wizara ya mambo ya nje ya Iran, kupokea rasmi malalamishi ya Iran. Nchini Yemen, Ndege za kivita za muungano unaongozwa na Saudi Arabia, zimefanya mashambulio zaidi ya anga dhidi ya wapiganaji wa Houthi katika maeneo ya Kaskazini, Kusini na kati kati mwa Yemen. Wapiganaji hao wa Houthi ambao wanapinga utawala wa rais Abd Rabbu Mansour Hadi, wamechukua uthibiti wa maeneo kadhaa nchini humo katika miezi ya hivi karibuni. Akiongea mjini Tehran, rais Rouhani alitaja mashambulio hayo kama makosa makubwa. Awali waziri wa mambo ya nje wa Marekani John kerry alionya Iran dhidi ya...

Kakobe Awataka Watanzania Kususia Kura Ya Maoni Kwa Madai Kuwa Katiba hiyo ni ya Kishetani

Image
  Akihubiri siku ya Pasaka katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship lililopo Mwenge katika Jiji la Dar-Es-Salaam, Askofu Mkuu Zachary Kakobe alisema kwamba, inajulikana wazi kwamba Lowassa amekuwa anautaka Urais kwa udi na uvumba kwa miaka mingi, hata mwaka 1995 alijitosa hadharani kuuwania, sasa anapodai kwamba hivi sasa kuna makundi yanayokwenda kwake kumshawishi agombee Urais, kana kwamba yeye hataki Urais, anakuwa anamdanganya nani? Ingawa katika mahubiri hayo ya saa mbili, Kakobe hakumtaja Lowassa kwa jina, hata hivyo Kakobe alisema, "Wako watu wengine ambao inajulikana wazi kwamba wamekuwa wakiutaka Urais kwa udi na uvumba, kwa miaka mingi, lakini hivi sasa wanasema kuna makundi ya watu yanawafuata nyumbani, kuwashawishi kugombea Urais; kama vile hawautaki Urais, hivi watu hawa wanamdanganya nani?   "Na wale wanaokwenda kumshawishi mtu ambaye kwa miaka mingi, anajulikana kwamba anautaka Urais, hawajui kwamba nao wanafanywa kuwa wajinga? Mtu anayejulik...

Wabunge 50 Kujiunga Na Chama Kipya Cha ACT-Tanzania

Image
  Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe amesema zaidi ya wabunge 50 wa vyama mbalimbali vya siasa nchini watajiunga na chama hicho kipya na kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.   Zitto ambaye alijivua ubunge wa Kigoma Kaskazini baada ya kufukuzwa uanachama wa Chadema, amebainisha kuwa wabunge hao, wakiwamo wa CCM na Chadema, ni miongoni mwa watu wanaokichangia fedha chama hicho kilichopata usajili wa kudumu Mei, mwaka jana na kuzinduliwa mwezi uliopita.   Pia, amewatangazia vita wabunge wa majimbo manane ya Mkoa wa Kigoma, akijigamba kuwa ili waweze kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo ni lazima wakubali kujiunga na ACT kwa kuwa chama hicho kimejipanga kuyabeba majimbo yote.   Akizungumza na Gazeti  la  Mwananchi  jijini  Dar es Salaam, Zitto alisema ACT ni chama kilichojipanga na ndiyo maana haikuwa ajabu katika mkutano wake mkuu wa hivi karibuni kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 400 na kufanya uz...

Shambulizi Garissa:Serikali yajitetea

Image
  William Ruto     Serikali ya Kenya imeitetea idara yake ya usalama kufuatia shutma kwamba ilichelewa kukabiliana na shambulio la chuo kikuu cha Garissa ambapo takriban watu 150 waliuawa. Shambulio hilo lilisitishwa baada wapiganaji wanne waliohusika kuuawa na maafisa wa polisi saa 15 baada ya kuvamia chuo hicho. Wanajeshi wa kenya    Lakini naibu wa rais William Ruto anasema kuwa kundi la kwanza la polisi liliwasili katika chuo hicho saa moja baada ya shambulizi. Amelipongeza jeshi la Kenya KDF kwa kile alichokitaja kua hatua za haraka.Lakini vyombo vya habari vimekuwa vikisema kuwa vikosi maalum vilivyowaua wapiganaji hao vilichelewa kufika katika eneo hilo kutokana na mfumo wa usafiri waliotumia. Wanajeshi wa kenya    Pia kuna madai kwamba maafisa wa polisi walifeli kuchukua hatua za dharura baada ya kupewa habari kwamba mmoja ya wauaji ambaye sasa ametambuliwa kama Abdirahim Abdullahi ni wakili na m...