Posts

Showing posts with the label habari za mastaa

Baada ya kuambiwa anaujauzito, Hii ndiyo picha aliyo post Aunt Ezekiel na kuandika haya

Image
Baada ya wengi kuongea na baadhi ya vyombo vya habari zikiwemo na blogs kuandika kuwa  Aunt Ezekiel  anaujauzito na hadi kufikia kudhaniwa ni nje ya ndoa pamoja na mmoja wa wanenguaji wa msanii  Diamond Platnumz  kuhisiwa anahusika, Masaa 24 yaliyo pita kupitia account yake ya instagram  Aunt Ezekiel  ameandika haya. Lazima ujue Kutofautisha kati ya Kitambi na Mimba Sasa hiki Chagueni wenyewe ni KITAMBI AU MIMBA!!!!!legoooooooooo......

Hemedy Kuja Na Video Mpya Jina Na Lini Inatoka Viko Hapa. #TwitZaMastaa

Image
Kama ilivyo kawaida kwa Hemedy Phd kutoa kazi na video mapema ili mashabiki wapate vyote kwenye radio na tv, Hii itatokea kwenye wimbo wake mpya GoodMorning. Video inatarajiwa kutoka December    

Soma alichoandika Masanja Mkandamizaji kuhusu uhusiano wa Wema na Diamond

Image
Masanja mkandamizaji mchekeshaji kutoka kundi la Komedi Orijino kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika mawazo yake juu ya uhusiano wa Wema Sepetu na Diamond. Hiki ndicho alichoandika,�Hili swala la diamond na wema nadhani mungu amemuhurumia mmoja wapo kati ya hao wawili. Kama wangekuwa watu wa kuoana wangesha oana uchumba gani mrefu kama wanasomea udokta???? Rafiki yangu nasib, kama kweli mlipendana kwa dhati hizo kasoro zinarekebishika, maana hakuna mwanadamu aliye sahihi kwan hata ww nasib unamapungufu yako. Na wewe dada yangu wema lazima ujue mme ndio kichwa cha nyumba kwa maelezo hayo inaonyesha haumsikilizagi mwenzio omba msamaha tenaaa na tena na ukubali kubadilika. Mi sipendi mkiwa mnaongozana wote kwenye ma show ya usiku mme kafanye kazi mke abaki home ukirudi mwili umepoa hata ujauzito unaingiaa!! Sasa woote stejini mkirudi miili ya moto si mtazaa popompoo jamaniii!! Nitafurahi kusikia tofauti zenu mmezimaliza kwa amani ili mashabiki wenu wasijisiki...

Inasemekana Hii Ndio Couple Mpya Ya Mastaa Duniani.

Image
Jennifer Lawrence Na Chris Martin Mpenzi wa habari za burudani duniani utakuwa umegundua trend inayoendelea kwa sasa ya couple nyingi za masta kuvunjika kwa sababu tofauti, Stori mpya ambayo imeenda tofauti ni kuhusu tetesi zilizosamba kuwa mwigizaji Jennifer Lawrence na kiongozi mwimbaji wa bendi ya rock ya Cold Play Chris Martin ni wapenzi. Vyanzo vingi vimeripoti kuwa tayari mashabiki wa watu hawa maarufu wamejumuisha majina yao na kuanza kuwaita �Martin Lawrence� . Ndoa ya Chris Martin ambaye ni rafiki wa karibu wa familia ya The Carters [Jay z Na Beyonce] ilivunjika miezi michache nyuma.

Star mwingine kutoka Tanzania ambaye page ya Facebook imekuwa verified

Image
Alama ya verified ndio inatambulisha ukurasa halali wa mtumiaji kwenye mitandao mingi sana. Alama hii ni muhimu sana hasa kwa watu maarufu wanaotumia mitandao ili kuepuka kuwepo kwa kurasa feki ambazo haziwahusu. Hivi sasa mtu maarufu ambaye page yake ya facebook imekuwa verified ni mchezaji wa kikapu kwenye timu ya Oklahoma City Thunders �Hasheem Thabeet�. Ukurasa wake wa twitter ulikuwa verified siku nyingi na hivi sasa mashabiki wake wa facebook watakuwa na uhakika kwasababu na facebook wame-verify ukurasa wake.

Picha 8 za Jumba la kifahari Oscar Pistorius alilopanga kuishi na mpenzi wake kabla ya kumuua.

Image
  Hizi ni baadhi ya picha Jumba kubwa la kifahari la Oscar Pistorius lenye thamani ya Paundi 530,000 ambalo alipanga kuhamia na mpenzi wake Reeva Steenkamp kabla ya tukio la kumpiga risasi akiwa bafuni ambapo kesi yake bado inaendelea. Pistorius tayari alikwishalipia nyumba hiyo baada ya makubaliano na mpenzi wake huyo baada ya kutembelea nyumba hiyo ambapo wapenzi hao waliwaambia marafiki zao juu ya mpango wa kuhamia katika nyumba hiyo jijini Johannesburg.