Posts

Showing posts with the label kitaifa

Kinachoendelea eneo la Mkwajuni baada ya wananchi kufunga barabara..Picha

Image
  Zoezi la Bomoabomoa leo lilikua likiendelea katika eneo la Mkwajuni, Dar es salaam , lakini safari hii wananchi waliobomolewa nyumba zao wameonekana kupandwa na hasira na kufunga barabara. Wananchi hao waliamua kuchoma matairi katikati ya barabara na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo hadi askari wa FFU walipoingilia kati. Hizi ni baadhi ya Picha kutoka eneo la tukio.

Hii Asilimia Ya Madini Ya Tanzanite Yanayotoroshwa Nje Ya Nchi Kila Mwaka.

Image
Asilimia 80  ya madini aina ya Tanzanite yanayozalishwa nchini Tanzania, yanatoroshwa nje ya nchi na wafanyabiashara wasio waaminifu, huku nchi ikiambulia asilimia 20 tu ya madini hayo yanayozalishwa eneo la Mererani mkoani Manyara. Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Masanja, amesema hayo wakati wa maonyesho ya kimataifa ya Vito, yanayofanyika jijini Arusha na kukutanisha washiriki zaidi ya 500, huku kampuni 69 zikishiriki maonyesho hayo. Masanja ametoa mfano wa mwaka 2013 ambapo Tanzania ilipata mapato yanayofikia dola za Marekani milioni 38 kutokana na Tanzanite, wakati Kenya walipokea Tanzanite yenye thamani ya dola milioni 100, huku India ikipata dola milioni 300 za madini hayo. Amesema kuwa kutokana na hali hiyo, serikali imeamua kujenga jengo la kuuzia madini hayo na litakapokamilika hakuna mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuuza madini hayo nje ya jengo hilo kama ilivyo sasa. Sammisago .com ndio mtandao wako kwa habari za burudani Afri...

Rombo Imetajwa Wilaya Inayongoza Kwa Ukatilia Wa Kijinsia Na Watoto Nchini Tanzania

Image
  Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania inaogoza kwa ukatilia wa kijinsia na watoto huku ikibainika kuwa watoto ndio wamekuwa wahanga wa kubwa katika jamii. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa Kilimanjaro Bi. Grace Limo wakati wa Uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani. Bi. Grace amesema watoto wengi katika wilaya hiyo wanathirika kwa kutumikishwa katika shughuli za kibiashara na kwa kuachishwa shule huku wengine wakilelea na wazazi ambao wamejikita kwenye ulevi wa Kupindukia.

Uliikosa picha aliyoiweka Rais Kikwete twitter baada ya kukutana na Wapinzani na alichoandika?

Image
Baada ya kukutana na viongozi wa vyamba mbalimbali vya upinzani Tanzania na kuzungumzia ishu ya bunge la katiba, iliamuliwa kwamba katiba ya zamani ndio itakayotumika kwenye uchaguzi mkuu ujao ila itafanyiwa marekebisho. Kwenye ukurasa wake wa twitter President JK ambae alikua hajaandika chochote toka Aug 6 2014, aliweka hiyo picha hapo juu ikimuonyesha kwenye mkutano na viongozi hao na kuandika >>  mabovu story .com ndio mtandao wako kwa habari za burudani Africa na nje, Tuwe pamoja huku pia  >> Instagram , Twitter Na Facebook

News kutoka bodi ya mikopo Tanzania kwenda kwa Wanafunzi elimu ya juu.

Image
  Bodi ya mikopo ya Wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania imeanzisha mpango mpya kwa ajili ya kupambana na uhaba wa Walimu wa masomo ya Sayansi na hesabu wa shule za msingi kwa kutoa mikopo kwa Wanafunzi wa ngazi ya stashahada (Diploma) watakaochaguliwa. Ni mpango maalum unaoanza mwaka huu wa masomo 2014/2015 ambapo Mkurugenzi msaidizi wa habari, elimu na mawasiliano Cosmas Mwaisobwa amesema huu mpango utasaidia Wanafunzi zaidi ya elfu tano. Maneno yake mengine ni haya >>> � Serikali inafanya jitihada za kuziba pengo la uhaba wa Walimu wa hayo masomo kwenye shule za msingi na sasa hii imekua programu maalum itakayoendeshwa na chuo kikuu cha Dodoma mwaka huu � Pamoja na hayo bodi imekiri kuchelewesha kuwalipa fedha za vitendo wanafunzi wa vyuo vitano mwezi July 2014 kutokana na changamoto ya uhaba wa fedha lakini ahadi ni kuwa malipo hayo yatafanywa hivi karibuni. Wanachuo hao ni kutoka Tumaini Makumira wanafunzi 1715, Stephano Moshi 1191, IFM 2578, M...

Kauli ya Jeshi la Polisi Tanzania juu ya viungo vya binadamu vilivyopatikana July 21.

Image
Kama mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii kuanzia usiku wa July 21 kulisambaa taarifa na picha zinazoonyesha viungo mbalimbali vya binadamu ambavyo vilitupwa katika daraja la Mpiji. Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni ameongea na Power Breakfast ya Clouds Fm na kusema>>�Kweli tumekwenda tumevikuta viungo mbalimbali vya binadamu kama mikono,miguu,vichwa na viungo vingine� �Lakini vipo ndani ya mifuko ya sulphet na iko mifuko kama 80 hivi lakini tumechukua viungo hivyo na kuvipeleka hospital ya Muhimbili kwanza kuhifadhi na kwa ajili ya uchunguzi Mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa� Bonyeza play kumsikiliza kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi kinondoni Kamilius Wambura

Matokeo ya Kidato cha 6 kama hujafanikiwa kuyaona yapo hapa.

Image
Baraza la mitihani la taifa leo limetangaza matokeo ya Watahiniwa wa Kidato cha 6,kama ulifanya mtihani wa kidato cha 6 basi waweza cheki matokeo hayo hapa hapa kwa mtu wako wa nguvu. NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA ACSEE 2014 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES   P0101 AZANIA CENTRE   P0104 BWIRU BOYS CENTRE   P0110 ILBORU CENTRE   P0112 IYUNGA CENTRE   P0116 KANTALAMBA CENTRE   P0119 KIBAHA CENTRE   P0123 KWIRO CENTRE   P0129 MARA CENTRE   P0132 MILAMBO CENTRE   P0133 MINAKI CENTRE   P0134 MOSHI CENTRE   P0136 MUSOMA CENTRE   P0140 MZUMBE CENTRE   P0143 NJOMBE CENTRE   P0144 NSUMBA CENTRE   P0145 NYAKATO CENTRE   P0147 PUGU CENTRE   P0150 SAME CENTRE   P0151 SENGEREMA CENTRE   P0152 SHINYANGA CENTRE   P0156 TANGA TECH. CENTRE   P0158 TOSAMAGANGA CENTRE   P0167 KIDUGALA SEMINARY CENTRE   P0184 AGAPE LUTH JUNIOR SEMINARY CENTRE   P0203 IRINGA GIRLS CENTRE ...

Na hii ni ya Benki kuu ya Tanzania tena baada ya kutangaza kuleta ile sarafu ya 500.

Image
Baada ya kuripotiwa kuwepo kwa mabadiliko ya noti ya sh. 500 ambayo itaacha kutumika siku chache zijazo nchini Tanzania na mbadala wake kuwa sarafu ya shilingi 500, Watanzania mbalimbali wamekuwa na wasiwasi na taarifa hiyo pamoja pia na kuamini uchumi wa nchi unaanguka. millardayo.com imepata nafasi ya kuongea na mchumi wa benki kuu kwenye kurugenzi ya utafiti na sera za uchumi Lusajo Mwankemwa ambae amejibu hizo headlines kwa kusema hiki kifuatacho. �Kwa niaba ya benki kuu ya Tanzania amewatoa hofu kuhusu haya mabadiliko na kusema haijaja kutokana na ukuaji na ushukaji wa uchumi wa nchi ya Tanzania, yaani kuanza kutumika kwa hii sarafu hakuhusiani na Tanzania kushuka kiuchumi� �Noti ya 500 imeonekana inachakaa sana ndani ya miezi 6 kutokana na kuwa na mzunguko mkubwa ikilinganishwa na noti nyingine na haipitii ule mfumo wa kawaida wa kibenki kurudi benki kuu kwa ajili ya kuibadilisha, tulitarajia Mwananchi anapokwenda bank kupeleka pesa zake basi na 500 iwe miongion...