Hii Asilimia Ya Madini Ya Tanzanite Yanayotoroshwa Nje Ya Nchi Kila Mwaka.

Asilimia 80  ya madini aina ya Tanzanite yanayozalishwa nchini Tanzania, yanatoroshwa nje ya nchi na wafanyabiashara wasio waaminifu, huku nchi ikiambulia asilimia 20 tu ya madini hayo yanayozalishwa eneo la Mererani mkoani Manyara.

Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Masanja, amesema hayo wakati wa maonyesho ya kimataifa ya Vito, yanayofanyika jijini Arusha na kukutanisha washiriki zaidi ya 500, huku kampuni 69 zikishiriki maonyesho hayo.

Masanja ametoa mfano wa mwaka 2013 ambapo Tanzania ilipata mapato yanayofikia dola za Marekani milioni 38 kutokana na Tanzanite, wakati Kenya walipokea Tanzanite yenye thamani ya dola milioni 100, huku India ikipata dola milioni 300 za madini hayo.

Amesema kuwa kutokana na hali hiyo, serikali imeamua kujenga jengo la kuuzia madini hayo na litakapokamilika hakuna mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuuza madini hayo nje ya jengo hilo kama ilivyo sasa.

Sammisago.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani Africa na nje, Tuwe pamoja huku

Comments

Popular posts from this blog

Where to get Free Games?

PES 2016 PS3 OPTION FILES