Kuhusu ushiriki wa Adam Kuambiana kwenye video ya Mdogo Mdogo ya Diamond Platnumz.
Ni kitu ambacho hakuna mtu ambaye aliwahi kuhisi au kutegemea kama Marehemu Adam Kuambiana ambaye alikua muongozaji[Director] wa filamu nyingi za Kitanzania kumbe nae kashiriki kwenye video ya Mdogo Mdogo.
Adam Kuambiana ambaye alifariki May 17 2014 wakati akiwa kambini kwa ajili ya filamu yake mpya ametajwa na Diamond kuhusika na utengenezaji wa Script[muongozo] wa video ya Mdogo Mdogo iliyotengenezwa South Africa na God Father.
�Nikawa nae studio nakumbuka nilikuwa nae studio kwa Tudd Thomas pale THT akawa anasikiliza wimbo akawa ananambia namna stori inavyotakiwa kwenda so naweza kusema stori inavyoanza picha hata ya kupata Stori ni Kuambiana ndiye aliyenipa.
Comments
Post a Comment