Ostaz Juma (kushoto) akiwa na mkewe Mariamu na mwanae Hayyat Mariamu Daudi Mtoto Hayyan Juma Ostaz Juma Namusoma Ostaz Juma akiwa Cape of Good Hope Baada ya usiri wa muda mrefu, bosi wa Mtanashati Entertainment, Ostaz Juma Namusoma ameamua kumuweka hadharani mkewe na mototo wake na hivyo kuzima zile tetesi kuwa Ostaz ni msela tu asiye na mke wala mtoto. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Ostaz Juma ameweka picha ya mkewe ajulikanaye kwa jina la Mariamu Daudi au mama Hayyan akiwa pamoja na mtoto wao wa kiume, Hayyan Juma. Sambamba na picha hizo, Ostaz alisindikiza na maneno yasemayo: �For those who didn't know that I have a wife and a kid, let it be known now...kwamba mimi nina mke na mtoto, nampenda sana mke wangu (mary david) na nampenda sana mwanangu hayyan boy hayyan juma. namuomba sana mungu atuhifadhi na maadui wa kibinadamu na wasio jua thamani ya familia ya mtu, eeh mola mjaalie mke wangu maisha marefu na afya na amani ya moyo wake na utulivu, utupe watoto weng...