TULIPENDANA KAMA PETE NA KIDOLE (1)
Ilikuwa kama kawaida yangu,nikitoka nyumbani kuelekea kazini,huwa napita kwenye baraza la kunywa kahawa,katika maeneo ya Buguruni kwa Mnyamani,kisha baada ya hapo naelekea kivukoni.Siku moja nilitoka nyumbani mapema sana,nikafika maeneo ya kunywa kahawa,majira ya saa moja Asubuhi.Watu wanaokunywa kahawa pale Mnyamani,walikuwa wakinifaham ,kwa jina la utani,kama JUNGU KUU" Muda huo,mzee chaurembo na Baba sikujua,walikuwa wamekwishafika kwenye kibaraza cha kahawa.Niliwasalimia na kuanza kunywa nao,kahawa.Mzee chaurembo,akamuliza Jungu kuu,hawajambo nyumbani?Jungu kuu akamjibu,Mke wangu hajambo.Baba sikujua akashtuka kidogo,na kumuliza Jungu kuu,mwenzio mzee chaurembo,amekuuliza nyumbani hawajambo?Lakini nashangaa ulivyomjibu kwamba,mke wako hajambo.Kabla jungu kuu ,hajamjibu Baba sikujua,Mzee chaurembo akadakia,unajuwa wewe Baba sikujua,ni kama jina lako,kama ungejua?usingeshangaa na kumuliza Jungu kuu.Mimi huyu ni jirani yangu,Jungu kuu namsifu sana,kwa sababu anajua kumpend...