Huyu dada nimemfahamu miaka mitatu iliyopita. Ni mwanasheria kwenye firm fulani jijini Dar, nilikuwa nina mpango wa kumuoa haraka, ila mmoja wa marafiki zake wa karibu aliniambia nijitahidi kumfahamu kwanza kabla sijaamua kumuoa nadhani alihisi kitu. Kufahamiana naye kwa muda tukaishia kupata mtoto mmoja wa kike ambaye sasa ana miaka miwili. Ni mwanamke mzuri sana, ni gumzo kila anapopita au kufanya kazi, hata nilitaka nitoane macho na patina mmoja wa firm yake. Kwa kweli anaita kila jicho ana mengi mazuri, lakini pia ana mapungufu yaliyonipigisha breki kali juu ya tope. Kwa sasa anaishi na wazazi wake, lakini mara nyingi saba tunalala kwangu. Nafahamika kwao kama mzazi mwenza, kwetu pia kaskazini wanamtambua. Amekuwa ni mwepesi sana wa kupata marafiki wa kiume, ana hasira za karibu, kujiachiachia sana kwa wanaume imekuwa sehemu ya maisha yake, yeye anadai si wapenzi wake. Wanataniana tu hii ni moja ya sababu iliyonizuia kumuoa. Nilihisi kama hajiheshimu.hayuko tayari kui...